Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi: Aziz KI agoma kuongeza mkataba Yanga

Aziz KI Mpira Tetesi: Aziz KI agoma kuongeza mkataba Yanga

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga raia wa Burkina Faso, Stephanie Aziz KI ameigomea timu hiyo kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo ya pale Jangwani.

Ikumbukwe mchezaji huyo alisajiliwa na Yanga tarehe 24/08/2022 akitokea Asec Mimosa ya nchini Ivory Coast ambapo alimaliza msimu akiwa na timu hiyo kama mchezaji bora wa msimu wa Ligi Kuu nchini humo.

Mara baada ya kutua yanga alisaini kandarasi ya miaka 2 kuitumikia timu hiyo kwa mshahara wa milioni 27 kwa mwezi na ada ya uhamisho wa dola laki mbili na nusu.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa, baada ya kuwa na msimu mzuri kwa kumaliza na mabao 10 na assist 7 msimu uliopita.

Aziz ameanza vyema msimu huu mpaka sasa ana goli 6 na assist 7, uongozi wa Yanga ulianza mazungumzo tangu juzi kumboreshea maslahi na kutaka kumuongezea mkataba tena wa miaka miwili ili asalie Jangwani hapo hadi 2026.

Mchezaji huyo anadaiwa kugoma kuhusu jambo hilo la kuongeza mkataba jambo ambalo limewafanya viongozi wa Yanga kukuna kichwa na kuwapa wasi wasi na hofu kubwa na kisha kujiuliza je anataka kwenda timu gani mchezaji huyo.

Kama ataweka msimamo huo, maana yake atalazimika kuondoka Yanga baada ya msimu huu kutamatika akiwa kama mchezaji huru na Yanga haitopata faida yoyote ile.

Chanzo cha karibu cha mchezaji huyo kikisema kuwa mchezaji huyo atabaki kucheza Tanzania msimu ujao lakini sio kwenye timu ya Yanga.

Swali ni, je, unahisi Aziz Ki atatimkia wapi kama hataki kubakia Yanga ila atabakia Tanzania akitumikia klabu nyingine?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live