Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetemeko la ardhi Morocco, Aziz Ki awatoa hofu Yanga

Aziz Kista Aziz Ki.

Sun, 10 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Yanga, Stephane Aziz Ki ambaye alikuwa na kikosi cha Timu ya Taifa ya Burkina Faso nchini Morocco katika mchezo wa mwisho wa kufuzu AFCON waliocheza juzi Ijumaa dhidi ya Eswatini, hajaathirika na tetemeko la ardhi lililotokea nchini humo, hivyo yupo salama.

Usiku wa kuamkia jana Jumamosi Septemba 9, 2023, imeripotiwa kutokea tetemeko la ardhi nchini Morocco na kuyakumba maeneo mbalimbali ya nchi hiyo ikiwemo Mji wa Marrakesh, Al-Haouz, Ouarzazate, Azilal, Chichaoua na Taroudant, huku vifo vingi vimeripotiwa kutokea maeneo ya miinuko na milima, huku takribani watu zaidi ya 153 wamejeruhiwa na vifo vikiripotiwa kufikia zaidi ya watu 296.

Burkina Faso juzi Ijumaa walikuwa na mchezo huo wa mwisho wa Kundi B kufuzu AFCON dhidi ya Eswatini ambao ulichezwa Dimba la Marrakech lililopo Marrakesh, Morocco na kumalizika kwa timu hizo kutofungana, huku Burkina Faso ikifuzu AFCON ikiwa kinara wa kundi hilo.

Akizungumzia hali yake na salamu zake za pole baada ya kutokea kwa tetemeko hilo la ardhi akiwa nchini Morocco, Stephane Aziz Ki alisema: “Nipo salama, sijaathirika na chochote kutokana na tetemeko hili, mimi ni mzima wa afya, watu waondoe hofu kabisa.

“Natoa pole kwa wale wote walioathirika na tetemeko hili, lakini pia pole iende kwa wananchi wote wa Morocco. Tupo pamoja nao kipindi hiki kigumu.”

Mpaka sasa zaidi ya watu 2000 wamepoteza maisha nchini Morocco huku wengine wengi wakijeruhiwa na wengine kupoteza makazi yao kutokana na tetemeko hilo. Hata hivyo juhudi za uokoaji zinaendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live