Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Tetemeko la Simba week’ kulikumba Taifa Julai 24

Simba Day Agosti 8 ‘Tetemeko la Simba week’ kulikumba Taifa Julai 24

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukisema Tamasha la Simba Day limeanza kuitetemesha Nchi utakuwa sahihi baada ya Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Simba kutoka kona mbalimbali nchini kujiweka tayari kwa mtoko huo.

Simba kwa kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania TRC wanatarajia kuzindua wiki ya Simba Jumatano ya Julai 24, mwaka huu ndani hifadhi ya Mikumi na kilele chake kitafanyika Agosti 3 mwaka huu katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika siku hiyo Simba itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya APR ya Rwanda. Viingilio vya Simba Day Mzunguko ni 5000, Orange 10,000, VIP C, 20,000, VIP B 30,000, VIP A 40,000 na tiketi za Platinum 200,000 tiketi ambazo zimeanza kuuzwa rasmi leo hii.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula, ameiambia spotileo kuwa wanazindua wiki ya Simba mkoani Morogoro katika mbuga ya Mikumi ili kuhamasisha zaidi utalii wa ndani pamoja na kukutanisha Simba SC na mnyama Simba wa hifadhini hapo.

“Klabu inajali wajibu wake kwenye Serikali tumeamua kutangaza utalii na kukuza uchumi wetu. Hatutaenda moja kwa moja katika hifadhi tutaanzania Morogoro katika matawi kisha kwenye hifadhi hizo,” amesema Kajula.

Ameongeza kuwa baada ya uzinduzi ya wiki ya Simba Morogoro, wataenda katika hifadhi hiyo ambayo ndani yake kuna uwanja wa mpira wa miguu na kucheza mechi ya kirafiki kati ya Simba ambapo msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba atakuwa sehemu ya kikosi cha wekundu hao wa Msimbazi dhidi ya wakazi wa Morogoro.

Nae Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema lengo la ushirikiano wa kuunganisha taasisi tatu ni kuboresha tamasha la Simba ambalo kilele chake itakuwa Agosti3, mwaka huu.

“Wiki ya Simba tunaenda kufanya uzinduzi Morogoro mjini baada ya hapo tutaenda Hifadhi ya Mikumu, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wanasimba lakini pia kuhamasisha watanzania na raia wakigeni kuja kufanya utalii nchini.

Kwa hali hiyo tumeamua kuwaambia Watanzania kuwa wanaweza kwenda kufanya utalii wa ndani kwa bei rahisi lakini tunatangaza bidhaa mpya wa SGR (Joshua Mutale), pamoja na kumuunga mkono wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan katika mradi huu,” amesema Ahmed.

Amesema Simba wamechukuwa mabehewa matatu, mawili yakiwa ya watu wa burudani akiwemo King Faida na Malaika Band na behewa la tatu litakuwa na watu wasipenda kelele lakini pia kutokana na maombi ya mashabiki wengi wameongeza behewa la nne.

Ameweka wazi taratibu ya wiki ya Simba, Julai 26, kutakuwa na droo ya makundi kwa ajili ya Julai 27 mwaka huu watakuwa na bonanza la Matawi yote ya Dar es Salaam kutafuta shabiki bora wa msimu litakalofanyika uwanja wa Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam.

“Julai 28 tutaenda Mbagala kwa ajili ya kumhamasisha kila mwanasimba, kila tawi wajikusanye pamoja waende kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji na kupata baraka zao kwa msimu mpya. amesema Ahmed.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirikia la Reli Tanzania,, Masanja Kadogosa amesema viongozi wa Simba wamefikiria kitu kizuri kwa sababu wanasapoti juhudi za Rais Samia kuchochea utalii wa ndani.

“Tutaenda Morogoro pamoja na tutarudi pamoja kwa kutumia Treni ya SGR, tutashirikiana na Simba kuhakikisha wanafanikisha jambo lao la kuzindua wiki ya Simba, Tukio la kuzalendo kwa nchi yao tunaanza kwa hiyo Simba inaweza kusaidia kututambulisha na naamini kwa ushirikiano huu tunatarajia kuona makubwa,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live