Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tete za Usajili leo Jumanne, Januari 17, 2023

Raphinha In Brazil Colours Winga wa Brazil Raphinha

Tue, 17 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Arsenal wamemfanya Declan Rice kuwa mlengwa wao mkuu wa uhamisho wa majira ya joto na wana imani kuwa wanaweza kushinda Chelsea ili kumsajili kiungo huyo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 24. (Times – usajili unahitajika)

Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund, Sebastian Kehl anapanga mazungumzo na kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham na wazazi wake kuhusu mustakabali wa kinda huyo mwenye umri wa miaka 19, na anasema hakujakuwa na ofa yoyote kwa ajili yake. (Kicker)

Winga wa Brazil Raphinha amekuwa akihusishwa na Arsenal, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 hana nia ya kuondoka Barcelona mwezi Januari. (Mundo Deportivo)

Newcastle United wanatazamia kuwasajili kiungo wa kati wa Chelsea wa Uingereza Conor Gallagher, 22, na hge, 26, pamoja na winga wa Morocco mwenye umri wa miaka 29, Hakim Ziyech mwezi huu. (Telegraph)

Mkurugenzi wa michezo wa RB Leipzig Max Eberl anasema “dalili ziko wazi” kwamba fowadi wa Ufaransa Christopher Nkunku, 25, atajiunga na Chelsea . (Bild, kupitia Mail)

Newcastle wamejiunga na Leicester City katika mbio za kumnunua fowadi wa Fiorentina na Argentina Nico Gonzalez, lakini klabu hiyo ya Serie A haitamruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kwenda kwa chini ya pauni milioni 40. (TuttoMercatoWeb)

Evertonna Newcastle wanafanya mazungumzo juu ya kumsajili mlinzi wa Bayer Leverkusen mwenye umri wa miaka 21 Piero Hincapie ambaye pia amekuwa akihusishwa na Tottenham. (Football Insider)

Beki wa Ufaransa h anasema “anafuraha” katika Arsenal wakati mazungumzo kuhusu mkataba mpya wa mchezaji huyo wa miaka 21 yakiendelea. (Independent)

Leeds United wameongeza dau lao la pauni milioni 22.2 kumnunua kiungo wa kati wa Angers Azzedine Ounahi, 22, ambaye aliivutia Morocco kwenye Kombe la Dunia la 2022. (90Minutes)

Chelsea na Tottenham hawamfukuzi tena mshambuliaji wa Everton Muingereza Anthony Gordon, 21. (CaughtOffside).

Brighton wanavutiwa na mshambuliaji wa Argentina mwenye umri wa miaka 24 Valentin Castellanos, ambaye yuko kwa mkopo Girona kutoka New York City. (Independent).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live