Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag sio kinyonge

Erik Ten Hag Media.jpeg Ten Hag sio kinyonge

Sun, 17 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ili kumfukuza kocha wao Erik Ten Hag, katika dirisha lijalo, Manchester United itatakiwa kutoa zaidi ya Pauni 10 milioni kwa ajili ya kumlipa kama sehemu ya fidia ya kuvunja mkataba wake.

Ajira ya Ten Hag kwenye kikosi cha Man United imeendelea kuwa kwenye hatihati kutokana ba matokeo ambayo timu hii imekuwa ikiyapata.

Kwa sasa inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi ikiwa kwenye hatari ya kutofuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kwa msimu ujao.

Ripoti zinaeleza, ikiwa Ten Hag atashindwa kuiwezesha timu hii kufuzu michuno ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao kuna uwezekano mkubwa sana akafukuzwa lakini tovuti ya The Times, inafichua kuwa haitokuwa rahisi kumvunjia mkataba.

Inaelezwa Man United inakumbana na changamoto kwenye masuala ya kifedha ambapo sheria zinawabana na ili kusajili kwanza wanatakiwa kuuza.

Hili ni moja kati ya mambo ambayo yanaonekana kutia ugumu mchakato wa kuvunjiwa mkataba Ten Hag.

Sababu ya kwanza inayoonekana kuweka ugumu kufukuzwa na Ten Hag ni kwamba anayetakiwa kutoa uamuzi wa kuondoka kocha huyo ni Sir Jim Ratcliffe mwenyewe.

Akifukuzwa itabidi alipwe Pauni 10 milioni, ambayo itatoka kwenye mfuko wa Ratcliffe ambaye pia atatakiwa kutoa fungu kwa ajili ya usajili wa dirisha lijalo.

Pia kigogo huyo atatakiwa kulipa zaidi ya Pauni 15 milioni kwa ajili ya kuvunja mkataba wa Dan Ashworth kutoka Newcastle United anayetakiwa ili ahudumu kama Mkurugenzi wa Mpira wa Miguu.

Mchakato wote huu utatumia pesa katika kipindi hiki ambacho ripoti zinadia bajeti haionekani kuwa upande wa Man United kutokana na sheria za matumizi ya pesa.

Chanzo: Mwanaspoti