Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag kumweka kitimoto Ronaldo leo

Ten Hag Kumshughulikia Ronaldo Leo Ten Hag kumweka kitimoto Ronaldo leo

Mon, 24 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Manchester United, Cristiano Ronaldo leo siku ya Jumatatu atakuwa kwenye kikao kizito na kocha wake, Erik ten Hag kujadili kile kilichotokea kwenye mchezo wao na Tottenham Hotspur huku taarifa zisizo rasmi zikisambaa kuwa klabu hiyo itamuonesha mlango wa kutokea kwenye dirisha la usajili la mwezi Januari.

Mustakabali wa Ronaldo bado haujulikani baada ya kocha Ten Hag kumtoa kwenye kikosi cha kwanza Mreno huyo huku kitendo chake kwenye mechi na Spurs kikionekana kumkera zaidi.

Ronaldo aliondoka kwenye uwanja wa Old Trafford kabla ya kipyenga cha mwisho cha mwamuzi kuhitimisha dakika 90, huku United ikiwa mbele kwa goli 2-0 dhidi ya vijana wa Antonio Conte siku ya Jumatano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live