Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag kuikamua Man Utd Milioni 15

Ten Hag Aomba Mashabiki Wa Man Utd Msamaha Kocha wa Man United, Erik Ten Hag

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: Dar24

Imefahamika kuwa, endapo Klabu ya Manchester United itaamua kuvunja mkataba wa Kocha Erik Ten Hag, basi italazimika kumlipa zaidi ya Pauni Milioni 15.

Ten Hag ambaye huu ni msimu wake wa pili ndani ya kikosi hicho, anaonekana kuwa na wakati mgumu kutokana na kupata matokeo yasiyoridhisha hadi sasa.

Wakati kukiwa na vuguvugu la Ten Hag kutaka kuvunjiwa mkataba wake kikosini hapo, Kocha wa Sporting Lisbon, Ruben Amorim na Zinedine Zidane, wanatajwa kuwa ndiyo mmoja atakuwa mrithi wake.

Ten Hag ambaye alitambulishwa ndani ya Man United Julai Mosi, 2022, mkataba wake unatarajiwa kufikia tamati Juni 30, 2025, hivyo amebakiwa na miaka miwili.

Wakati Ten Hag akiwa katika wakati mgumu kikosini hapo, imeripotiwa kwamba, baadhi ya wachezaji wa Man United hawapendezwi na namna kocha huyo anavyowafanyia Jadon Sancho na Hary Maguire.

Maguire amekuwa hana nafasi kubwa ya kucheza kikosini hapo huku mwanzoni mwa msimu huu akivula kitambaa cha unahodha na kukabidhiwa Bruno Fernandes.

Kwa upande wa Sancho, miezi kadhaa nyuma, aliwekwa kando na kocha huyo ambapo amemuondoa kwenye program zake za mazoezi.

Chanzo: Dar24