Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag kuamua wa kuondoka na kubaki Man United

Ten Hag Aomba Mashabiki Wa Man Utd Msamaha Ten Hag kuamua wa kuondoka na kubaki Man United

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Manchester United kinaweza kuonekana tofauti sana mwakani - huku wachezaji nane wakiwa tayari kuondoka Old Trafford itakapofika Juni 2024.

Vijana wa Erik ten Hag wameanza msimu huu kwa tabu sana na sasa wako nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, pointi saba nyuma ya vinara Manchester City ambao ni mabingwa watetezi.

Pia mashetani wekundu wapo hatarini kutolewa kwenye michuano ya Ligi Mabingwa baada ya vichapo vitatu kati ya mechi nne walizocheza hatua makundi, huku mwekezaji Sir Jim Ratcliffe akitarajiwa kuchukua timu kwa asilimia 25 mchakato utakapokamilika.

Sasa kutokana na mchakato huo kuna baadhi wa wachezaji wanaweza kuondolewa huku wachezaji kama Aaron Wan-Bissaka, Victor Lindelof, Anthony Martial, Hannibal Mejbri, Jonny Evans na Tom Heaton wote wanakaribia mwisho wa mikataba yao.

Haijulikani kama kiungo anayekipiga kwa mkopo Sofyan Amrabat na Sergio Reguilon watapewa mikataba ya kudumu.

Hapa, kwa mujibu wa Mirror imetoa tathmini ya wachezaji ambao Ten Hag anatakiwa kufanya maamuzi nani anastahili kuondoka au kubaki.

Aaron Wan-Bissaka

Man United wana chaguo la kumwongeza mkataba beki huyo kwa mwaka mmoja zaidi. Beki huyo wa kulia anakaribia kufikisha umri wa miaka 26 mwezi ujao, yuko vizuri kulingana na umri wake na amekuwa na mchango kwa klabu.

Bissaka amerejea baada ya kupona majeraha na imekuwa ahueni kwa kocha wake ambaye anakibiliwa na wachezaji majeruhi wengi msimu huu.

Ikizingatiwa Wan-Bissaka aligharimu Pauni 50 milioni alipowasili akitokea Crystal Palace miaka minne na nusu iliyopita, itakuwa jambo la kushangaza ikiwa United ingefuta uwekezaji huo mkubwa. Kuna uwezekano Bissala akapewa mkataba mpya.

Victor Lindelof

Man United pia inaweza kuongeza mkataba wa Lindelof kwa mwaka mwingine. Uamuzi huu ni mgumu zaidi kwani atafikisha miaka 30 Julai mwakani lakini hakuwahi kuwa beki tegemeo wa kati tangu msimu uliopita na mara nyingi Lisandro Martinez na Raphael Varane ndo wamekuwa wakicheza, lakini msimu huu Harry Maguire anaonekana kuchukua nafasi kubwa lakini Ten Hag bado anamkubali. Amejumuishwa katika mechi zote isipokuwa mbili za Ligi Kuu Emgland  msimu huu.

Lindelof hana uwezekano wa kupata mkataba mpya mrefu, lakini kuongeza mkataba kwenye kipengele chake ni jambo la busara, kwani kunaipa United muda wa kuamua juu ya mustakabali wake wa muda mrefu.

Sofyan Amrabat

Mengi yalitarajiwa kutoka kwa Amrabat kutokana na kiwango chake kwenye fainali za Kombe la Dunia Qatar, alipoisaidia Morocco kufika nusu fainali kwa mara ya kwanza. Ten Hag, ambaye alimfundisha mchezaji huyo huko Utrecht, alifurahi alipomsajili kwa mkopo dirisha la kiangazi, Man United iliilipa Fiorentina ada ya mkopo ya Pauni 8.6 milioni na inaweza kumsajili kwa mkataba wa kudumu Julai mwakani kwa Pauni 17.1 milioni pamoja na nyongeza ya Pauni 4.2 milioni. Hata hivyo, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 bado hajaonyesha makali yake lakini ana nafasi ya kumshawishi Ten Hag na kununuliwa jumla.

Sergio Regulion

Ni ngumu kufikiria kama Regulion atabaki Man nited hadi kipindi cha usajili wa kiangazi. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alijiunga kwa mkopo akitokea Tottenham kuchukua nafasi ya Luke Shaw ambaye alipata majeraha ya muda mrefu sambamba na Tyrell Malacia. Beki huyo alisajiliwa saa chache kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Sasa kwa mujibu wote Shaw na Malacia wanatarajia kurejea hivi karibuni, jambo ambalo huenda Regulion  akafanya maamuzi ya kudondoka.

Hannibal Mejbri

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 alifanya vizuri alipokuwa akikipiga kwa mkopo Birmingham City msimu uliopita na tayari amejumuishwa mara 27 kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tunisia.

Kiungo huyo ana uwezo wa kucheza soka lakini hapati nafasi ya kucheza chini ya chini ya Ten Hag - Katika mechi sita za mwisho za ligi alisugua benchi jambo ambalo limempa wakati mgumu.

Huenda ni wakati wa Hannibal kuwasilisha ombi la uhamisho itakapofika dirisha dogo la usajili, lakini Man United wana chaguo la kuongeza mkataba wake kwa miezi 12 zaidi chaguo ambalo watalitumia kuhakikisha haondoki bure lakini anahitaji kupata nafasi zaidi ya kucheza ili kujihakikisha hatma yake Old Trafford.

Anthony Martial

Hakika hatma ya Martial ndani ya viunga vya Old Trafford imekwisha. Mfaransa huyo, ambaye atatimiza umri wa miaka 28 mwezi ujao, huwa anapata nafasi mara chache lakini lengo lake ni kupata nafasi ya kudumu. Man United inaweza kuongeza mkataba wake kwa miezi 12 zaidi, lakini anachotakiwa ni kuongeza juhudi kila akipewa nafasi ya kucheza pengine mabosi wanaweza kumfikiria akabaki. Straika huyo alikuwa hatari miaka kadhaa iliyopita lakini sasa kiwango chake kimeshuka.

Jonny Evans

Beki huyo mkongwe alirejea Man United kwa usajili wa kushtukiza siku ya mwisho ya dirisha usajili la kiangazi na amekuwa nyongeza muhimu kwenye kikosi cha Ten Hag, akicheza mechi tano za Ligi Kuu England. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ireland Kaskazini anatimiza umri wa miaka 36 mwezi Januari na atahitajika kuendelea kucheza ikiwa anataka mkataba mwingine wa miezi 12. Hivi sasa, ni ngumu kuhukumu kwani anakabiliwa na majeraha aliyopata kwenye mechi dhidi ya Luton City.

Tom Heaton

Ukizungumzia wachezaji wakongwe Man United huenda Heaton akajumuishwa endapo atapewa mkataba mwingine abaki Old Trafford. Kipa huyo wa zamani wa England, ambaye atafikisha umri wa miaka 38 mwezi Aprili, anatoa uzoefu wa kutosha na yuko tayari kuziba nafasi ya Andre Onana au Altay Bayindir iwapo itatokea wamepata majeraha.

Bado Heaton anaweza kuendelea kuwa Old Trafford kwa miaka miwili au mitatu ili kupata nafasi ya kucheza wiki kwa wiki. Alihusishwa kutakiwa na Luton City wakati wa dirisha la uhamisho lililopita na huenda akatamani changamoto mpya ifikapo Juni. Usishangae kipa huyo akiondoka Old Trafford.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live