Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag katoa masharti Man United

'Huu Ni Mwisho Wa Ten Hag   Hakuna Kurudi Nyuma' Ten Hag katoa masharti Man United

Fri, 14 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ikiwa ni siku chache baada ya kuripotiwa kwamba kocha wa Manchester United, Erik ten Hag ataendelea kubakia kwenye kikosi hicho, ripoti zinadai ametoa masharti kwa wamiliki wa timu hiyo wanaohitaji kumuongeza mkataba mpya.

Man United imeamua kuendelea kusalia na Ten Hag baada ya majadiliano ya muda na imepanga kumwamini aiongoze timu hiyo kwenye nchi ya ahadi.

Inaelezwa Man United imempa kocha huyu ofa ya mkataba wa miaka mitatu utakaomalizika mwaka 2027, lakini Mholanzi huyo amekataa kusaini hadi ahakikishiwe mambo matatu makubwa.

Sharti la kwanza ni kutoingiliwa kwenye masuala ya kiufundi, ambapo katika mechi za mwisho msimu uliopita mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo Jason Wilcox alikuwa akifanya hivyo ingawa kuna muda suala hilo lilikuwa likizaa matunda kwani alipendekeza Bruno Fernandes achezeshwe kama namba tisa wa uongo katika mchezo wa fainali ya Kombe la FA na akacheza vizuri sana.

Vilevile Ten Hag anataka Jadon Sancho asirudi kwenye kikosi hadi pale atakapokuwa tayari kuomba msamaha baada ya kutamka hadharani kwamba yeye ni mwongo.

Sharti la tatu ni kutaka kocha wake wa washambuliaji Benni McCarthy kupewa mkataba mpya wa kuendelea kuhudumu kwenye timu hiyo wakati ule wa sasa ukitarajiwa kumalizika ndani ya wiki chache zijazo.

Man United ilikuwa inasita kumwongeza Benni ambaye ni raia wa Afrika Kusini mkataba mpya kwa sababu haikuwa imemua hatma ya Ten Hag.

Ukiondoa masharti hayo matatu ya Ten Hag, mabosi walimuomba kwamba asiwe na mamlaka kwenye masuala ya usajili na kazi hiyo iachwe kwa kamati maalum, Ten Hag amekataa na kusisitiza usajili wote ataufanya mwenyewe.

Vilevile Ten Hag katika mkutano na tajiri Jim Ratcliffe amemtaka kigogo huyo kuamini kazi ya benchi la ufundi na kuwasapoti kwani anaona hapati sapoti ya kutosha kutokwa kwa bosi huyo.

Ten Hag na vijana wake, wataanza mechi za kujipima ubavu kama sehemu ya maandalizi ya msimu mpya Julai 15, watakapovaana na Rosenborg huko Norway kabla ya kutua Scottland kuvaana na Rangers kwenye dimba la Murrayfield siku tano baadaye.

Kisha itafanya safari kwenda Marekani ambako itakutana na Arsenal, Real Betis na baadaye kuwavaa mahasimu Liverpool.

Akizungumzia maandalizi ya msimu ujao, Ten Hag amesema: ”Maandalizi ya msimu ni kipaumbele chetu kwa sasa, ni muda pekee ambao unakuwa na timu kwa pamoja, hivyo unaweza kuitengeneza vile unavyohitaji. Tutakuwa imara kadri iwezekanavyo, ingawa tutawakosa wachezaji wetu watakaokwenda kuyatumikia mataifa yao kwenye mashindano ya Copa America na Euro.

Chanzo: Mwanaspoti