Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag awatibua mabosi wake

Sir Jim Ratcliffe Ew Ten Hag awatibua mabosi wake

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Erik ten Hag huenda akawekwa kitimoto na mabosi wa Manchester United baada ya kuweka hadharani yaliyojiri kwenye kikao chao cha siri kilichofanyika Ibiza hivi karibuni.

Kocha huyo wa Man United alikwenda mapumziko huko Ibiza, ndipo mabosi wa Man United walimfuata na kumwambia ataendelea kubaki kuongoza benchi la ufundi la miamba hiyo ya Old Trafford.

Mabosi wa Man United walimwambia Ten Hag walifanya mchakato wa kuchukua kocha mwingine, akiwamo kocha wa zamani wa Chelsea na Bayern Munich, Thomas Tuchel, lakini mwisho wamefanya uamuzi wa kubaki na huduma yake.

Kinachoelezwa ni Ten Hag hakuwa akifurahishwa na namna mabosi wa Man United wanavyomfanyia, hivyo aliamua kwenda zake likizo bila ya kutambua hatima ya kibarua chake kwenye kikosi hicho kipoje baada ya kuwapo kwa taarifa angefunguliwa mlango wa kutokea baada ya timu hiyo kumaliza nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu England msimu uliopita.

Kinachoelezwa ni mmiliki mpya wa klabu hiyo, bilionea Sir Jim Ratcliffe na wasaidizi wake hawakufurahishwa na uamuzi wa Ten Hag kuweka hadharani ishu za mkutano wao, kwa kuwa wao walidhani hayo yalikuwa mazungumzo ya siri.

Mabosi wa Man United wanamtaka Ten Hag, 54, asaini mkataba wa miaka mitatu, lakini dili hilo bado halijafikiwa makubaliano ya mwisho.

Bilionea Ratcliffe anamiliki asilimia 27.7 ya hisa kwenye kikosi hicho na majukumu yake ni kusimamia oparesheni zote za maendeleo ya soka.

Yeye na msaidizi wake Sir David Brailsford wamemwaajiri Jason Wilcox, ambaye atakuwa mkurugenzi wa ufundi.

Wakati huo, mkurugenzi wa soka Dan Ashworth na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu, Omar Berrada watatua watakapoachana na klabu zao za zamani Newcastle United na Manchester City mtawalia. Man United itacheza Europa League msimu ujao na mchezo wao wa kwanza kwenye pre-season utakuwa Julai 15, watakapokipiga na Rosenborg ya Norway huko Trondheim.

Chanzo: Mwanaspoti