Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag awasilisha majina manne hatari Man United yumo huyu ..!

Southgate Anadokeza Kuhusu Kuanza Kwa Toney Kwenye Euro 2024 Mshambuliaji wa klabu ya Brentford Ivan Toney

Wed, 12 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benchi la ufundi la Manchester United chini ya kocha Erik ten Hag limependekeza majina ya washambuliaji zaidi ya wanne ambao inahitaji mmoja wao asajiliwe katika dirisha hili na miongoni mwa majina hayo ni straika wa Brentford na England, Ivan Toney, 28, pamoja na Jonathan David anayeicheza Lille na timu ya taifa ya Canada.

Mastaa hawa wamekuwa kwenye rada za timu nyingi barani Ulaya kutokana na viwango bora walivyoonyesha misimu uliopita.

Man United pia imewekeza nguvu kubwa katika kuhakikisha wanamsajili mshambuliaji mmoja kati ya Jonathan ama Toney kwa sababu inaona kwamba itawapata kwa bei rahisi.

Katika msimu uliopita Toney alifunga mabao manne katika mechi 17 za michuano yote, wakati Jonathan akifunga mabao 26 katika mechi 47 za michuano yote.

Toney alikosa sehemu kubwa ya msimu uliopita kutokana na kutumikia adhabu ya kufungiwa kujihusisha na masuala ya soka kutokana na kesi ya kujihusisha na mchezo ya kubashiri matokeo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live