Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag awashitukia mastaa wanaojivunja

Erik Ten Hh Ten Hag awashitukia mastaa wanaojivunja

Thu, 20 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Erik ten Hag anaamini presha ya kuichezea Manchester United imefanya baadhi ya mastaa wake kutumia muda mwingi kwenye chumba cha matibabu kwa madai ni wagonjwa wanaosumbuliwa na maumivu mbalimbali.

Man United ilikabiliwa na majeruhi wengi sana kwenye kikosi chake msimu uliopita na hivyo kujikuta wakimaliza nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, nafasi ya chini zaidi kuwahi kushika kwenye historia yao katika michuano hiyo.

Kocha huyo wa Old Trafford anaamini kuna baadhi ya wachezaji wake walikuwa hawana uwezo wa kuhimili kukosolewa kila wakati timu hiyo inapocheza na jambo hilo limewafanya wengi kujifanya ni majeruhi ili wasitumikie timu.

Ni presha kubwa kwa mchezaji yeyote anayevaa jezi ya Man United na hasa ukizingatia kwamba timu inapokuwa haina matokeo mazuri uwanjani.

Jambo hilo limefanya wachezaji wengi kujiondoa kwenye presha ya kucheza mechi ili kuepuka lawama.

Ten Hag amekuwa akiwatetea wachezaji wake kutokana na kuwa majeruhi, lakini kinachoonekana kwenye maelezo yake, anafahamu tatizo ni nini.

Hata hivyo, licha ya kushindwa kufichua tatizo ni nini hasa, kocha huyo anaamini presha imechangia kwa kiasi kikubwa kwa wachezaji kujifanya wagonjwa na kushindwa kutumikia timu jambo ambalo limekuwa na madhara makubwa kwenye matokeo yao ya uwanja.

Maneno ya Ten Hag yanakazia yale ya kocha wa zamani wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer, aliyewahi kusema kwenye kikosi cha timu hiyo kuna wachezaji wengi sana waoga.

Man United ilikuwa na kesi 64 tofauti za majeruhi kwa msimu uliopita.

Jambo hilo lilimfanya kocha Ten Hag kulazimika kutumia kombinesheni 30 tofauti ya wachezaji kwenye beki ya kati.

Kulikuwa na wachezaji 11 waliokosa mechi ya ugenini dhidi ya Crystal Palace, lakini kwenye mechi ya fainali ya Kombe la FA, ambayo ilikuwa ya mwisho kwao kwa msimu uliopita, majeruhi walikuwa watatu tu.

Straika Anthony Martial alikuwa mmoja wa wachezaji walikuwa wakitafuta kisingizio cha kuwa majeruhi, lakini kiukweli staa huyo hakuwa na majeraha makubwa ya kihivyo.

Chanzo: Mwanaspoti