Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag atatoboa?

Erik Ten Hag Media.jpeg Ten Hag atatoboa?

Sun, 24 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ndo hivyo, moja ya maswali ambayo mashabiki wengi wa soka wanajiuliza ni ikiwa kocha wa Manchester United, Erik Ten Hag atavuka mwaka 2023, salama kutokana na matokeo ambayo timu yake imekuwa ikiyapata.

Man United leo imepoteza dhidi ya West Ham ugenini kwa mabao 2-0 na kuifanya iwe kwenye nafasi ya nane ikiwa na pointi 28, huku ikiwa haijapata ushindi kwenye mechi tano mfululizo za michuano yote.

Huu unakuwa ni muendelezo wa rekodi mbovu za timu hii kwa msimu huu ambapo imetolewa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa, Carabao na imeendelea kufanya vibaya kwenye muendelezo wa ligi hiyo.

Mtihani mkubwa upo kwa Ten Hag ambaye anaonekana kukalia kuti kavu ikiwa timu itaendelea kupata matokeo mabaya, huenda akafungashiwa virago na tayari majina ya makocha kadhaa wanaoweza kuchukua nafasi yake wameshaanza kutajwa na miongoni mwao ni Kocha Aston Villa, Unai Emery.

Mechi ijayo, Man United itacheza dhidi ya Aston Villa inayoonekana kuwa na kiwango bora ambapo hadi sasa inashikilia nafasi yapili baada ya kucheza mechi 18 na kukusanya alama 39.

Chanzo: Mwanaspoti