Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag ataka kujua hatma yake Man United

Man Utd 'moja Ya Timu Zinazoburudisha' Ligi Ya Premia   Ten Hag Ten Hag achukizwa mambo kuchelewa

Mon, 10 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ndo hivyo. Kocha Erik ten Hag ameripotiwa kutokuwa na furaha kutokana na mambo kucheleweshwa juu ya kufahamu hatima ya kibarua chake kwenye kikosi cha Manchester United.

Kocha huyo Mdachi msimu wake wa pili kwenye kikosi cha Man United haukuwa mtamu baada ya timu hiyo kukusanya pointi chache zaidi kwenye Ligi Kuu England.

Man United ya Ten Hag, 54, ilishindwa kufuzu michuano yoyote ya Ulaya kwa msimu ujao kupitia ligi, hivyo ilihitaji kushinda Kombe la FA ili kukamatia tiketi ya kucheza Europa League msimu ujao.

Mabosi wa Man United wameripotiwa kufanya tathmini ya msimu wao ulivyokuwa kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho wa kuhusu kocha.

Lakini, sasa Ten Hag anavurugwa kwa kitendo cha mabosi hao wa Man United kushindwa kumweka wazi mapema juu ya hatima yake.

Awali ilielezwa kwamba kilichokuwa kikisubiriwa ni fainali ya Kombe la FA huko Wembley, ambayo imeshafanyika na wiki kadhaa zimeshapita sasa, lakini mabosi wa juu wa klabu hiyo bado hawajaamua kuhusu kocha huyo kama ataendelea kubaki au atafunguliwa mlango wa kutokea.

Kinachosubiriwa kwa sasa ni mmiliki mpya wa miamba hiyo ya Old Trafford, Sir Jim Ratcliffe kufanya uamuzi wa mwisho juu ya hatima ya kocha huyo, huku makocha wengine wanaohusishwa na timu hiyo ni pamoja na makocha wa zamani wa Chelsea, Mauricio Pochettino na Graham Potter.

Kocha wa England, Gareth Southgate, ambaye ni shabiki mkubwa wa tajiri Ratcliffe yumo kwenye orodha, lakini akisubiri kuona majaaliwa ya kikosi chake cha Three Lions Euro 2024.

Chanzo: Mwanaspoti