Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag asema wachezaji walikuwa 'wazembe' kipigo cha Spurs

Ten Hag Asema Wachezaji Walikuwa 'wazembe' Kipigo Cha Spurs Ten Hag asema wachezaji walikuwa 'wazembe' kipigo cha Spurs

Sat, 26 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Meneja wa Manchester United Erik ten Hag amewashutumu wachezaji wake kwa kutokimbia vya kutosha katika mechi ya kushindwa kwao na Tottenham.

United ilipoteza kwa mabao 2-0 siku ya Jumamosi dhidi ya Spurs na Ten Hag alilaumu safu ya ushambuliaji na ulinzi ya United.

Mholanzi huyo aliongeza kuwa wachezaji wake bila shaka walikuwa wameshuka chini ya viwango anavyodai.

"Hawakukimbia, au walikimbia kwa wakati mbaya, wakiwa wamechelewa sana. Hawafanya bidii - hasa mbele," alisema.

"Niliwapa maoni yangu kuwa hili halikubaliki. Kila mtu lazima awajibike. Tunahitaji wachezaji wanaowajibika."

Mwanzoni mwa msimu uliopita aliwaita wachezaji siku yao ya mapumziko kukimbia maili 8.5 baada ya timu hiyo kufungwa magoli 5-0 na Brentford.

Kulingana na Ten Hag, kiwango cha mchezo wa United dhidi ya Tottenham kilishuka baada ya takriban dakika 35, ambapo nahodha Bruno Fernandes alipoteza nafasi nzuri ya bao la wazi.

Chanzo: Bbc