Kocha Mkuu wa Manchester United, Erik ten Hag, amepuuzia kuzomewa na mashabiki kwa uamuzi wake wa kumtoa Rasmus Hojlund wakati wa kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Brighton, juzi Jumamosi (Septemba 16).
Siku mbaya kwa Ten Hag ilifanywa kuwa mbaya zaidi wakati uamuzi wake wa kumtoa Hojlund na kumwingiza Anthony Martial katika kipindi cha pili ulichochea sauti kubwa kutoka kwa mashabiki.
“Nadhani ilikuwa nzuri,” alisema Ten Hag.
“Unaona mashabiki katika dakika ya kwanza pale Old Trafford, mapokezi ya (Hojlund) yalikuwa mazuri. Nadhani alifanya vizuri sana. Ni vema wakatoa ishara hii, ujumbe huu. Itampa Rasmus imani.”
Højlund mwenye umri wa miaka 20 nusura aweke mechi yake ya kwanza United kwa kufunga bao, lakini akapata bao la kusawazisha kipindi cha kwanza lililokataliwa na VAR.
Mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 72 majira ya joto alilazimika kusubiri kucheza mechi yake yå kwanza baada ya kuwasili kutoka Atalanta akiwa na jeraha la mgongo na Ten Hag alisema hakuwa na uwezo wa kucheza dakika zote 90 dhidi ya Brighton.
“Kila mtu anajua alikuja na suala dogo,” aliongeza.
“Tulimjenga kwa muda wa wiki tatu au nne zilizopita, lakini hayuko tayari kwa mchezo mzima na tuna michezo mingi ya kucheza kwa muda mfupi, kwa hivyo lazima tujitengenezee.
“Iwapo atajeruhiwa kwa sababu hana uwezo wa kucheza dakika 90 basi tuko mbali sana kuliko tunakotaka kuwa.”