Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag anataka mshambuliaji mpya dirisha la usajili lijalo

Ten Hag Anataka Mshambuliaji Mpya Dirisha La Usajili Lijalo Ten Hag anataka mshambuliaji mpya dirisha la usajili lijalo

Sat, 13 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Mkufunzi wa Manchester United Erik ten Hag anataka kusajili mshambuliaji katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi.

Mholanzi huyo alihisi chaguo lake la mabao kwa msimu huu "lingetosha".

Lakini kukiwa na mechi saba za Ligi Kuu England, United wana mabao 45 pekee, ikiwa ni timu chache kati ya 10 bora.

Alipoulizwa katika mkutano wa wanahabari jinsi itakavyokuwa muhimu kumleta mfungaji aliyethibitishwa Old Trafford msimu huu wa joto, Ten Hag alisema: "Nadhani ingesaidia."

Kwa kweli, anataka zaidi ya mpinzani mmoja hodari kwa kila jukumu kwenye timu.

Ten Hag aliongeza: "Unahitaji chaguo zaidi. Unahitaji nafasi mbili katika kila nafasi.

"Baadhi ya nafasi ambazo hatukuwa na chaguo msimu huu - nafasi ya mshambuliaji, nafasi ya beki wa kushoto - na hiyo ina athari mbaya kwa matokeo."

United, ambao watasafiri kumenyana na Bournemouth Jumamosi,walimsajili mshambuliaji wa Denmark Rasmus kutoka Atalanta kwa £72m kwa mkataba wa miaka mitano Agosti mwaka jana.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ndiye mfungaji bora wa klabu hiyo katika kampeni yake ya kwanza akiwa na mabao 13 katika mechi 34 alizocheza katika mashindano yote.

Mshambulizi wa Uingereza, Marcus Rashford ametikisa nyavu mara nane katika mechi 38 huku mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa, Anthony Martial, ambaye yuko nje tangu kufanyiwa upasuaji wa kinena mwezi Januari, amefunga mara mbili katika mechi 19 alizocheza.

Chanzo: Bbc