Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag anashindwa wapi kumtumia Scott McTominay?

GettyImages 1285360934 Scott McTominay

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Scott McTominay akivaa uzi wa timu ya taifa ya Scotland anakuwa "Prime Frank Lampard" mpaka unajiuliza ana pacha wake nini pale Man United.

Ndio mchezaji aliehusika na mabao mengi kwenye Euro Qualifiers akiwa na mabao 6 na assisti 1 tena akiwa amepiga mashuti 7 tu yaliyolenga goli.

Yani Scott akilenga lango akiwa na Uskochi 98% mpira unautoa wavuni. Alafu uwezo wa Scott kupiga mpira kwa nguvu na ukabaki chini (Low Shot Technique) ni moja ya technique zake bora ambazo hazizungumzwi kabisa.

Hajachelewa sana na naamini akipata timu au akitumika kiusahihi tunaweza tukawa tunamwangalia Box to Box Mid mzuri hapo mbeleni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live