Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag amkingia kifua Bruno Fernandes

Ten Hag X Bruno.jpeg Ten Hag amkingia kifua Bruno Fernandes

Wed, 8 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amesema kua kiungo wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Ureno Bruno Fernandes ataendelea kusalia kama nahodha wa klabu hiyo licha ya maneno yanayoendelea.

Taarifa zimeenea siku za karibuni kua kiungo huyo anaweza kuondolewa kua nahodha msaidi ndani ya klabu ya Manchester United, Lakini kocha Ten Hag ameweka wazi kua kiungo huyo ataendelea kua nahodha wa timu hiyo na hayo ambayo yanaendelea hayana nguvu ndani ya timu hiyo.

Kocha huyo wakati anazungumza na wanahabari kuelekea mchezo wao wa Europa league dhidi ya Real Betis na kusema ana furaha na kiungo huyo kuendelea kua nahodha wa klabu hiyo kwa kushirikiana na Harry Maguire na kusema kiungo huyo anafanya kazi kubwa ndani ya timu hiyo.

Kocha Ten Hag ameonesha kuvutiwa na kiwango ambacho anakionesha Bruno Fernandes ndani ya msimu huu, kwani mchezaji huyo amekua akijitoa kwa kiwango kikubwa kwajili ya kuisaidia klabu hiyo hivo kocha huyo anaona kiungo huyo anafaa kuendelea kua kiongozi kwenye timu hiyo.

Bruno Fernandes ameibua maneno kwa mashabiki wa klabu hiyo siku za hivi karibuni baadhi yao wakitaka avuliwe unahodha ndani ya timu hiyo, Lakini kutokana na uimara wake ndani ya timu hiyo kocha Ten Hag anaona kiungo huyo bado anaendelea kua kiongozi ndani ya timu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live