Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag amfungulia geti Victor Lindelof

Victor Lindelof Victor Lindelof

Wed, 19 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag yupo tayari kumfungulia milango ya kutokea beki wa kati Victor Lindelof baada ya kuripotiwa kuwapo kwenye rada za Jose Mourinho, anayemtaka akakipige kwenye kikosi cha Fenerbahce huko Uturuki.

Beki huyo raia wa Sweden, Lindelof alitua Old Trafford mwaka 2017, wakati huo Man United ilipokuwa chini ya kocha Mourinho na kwenye kikosi hicho amecheza zaidi ya mechi 250.

Man United ililipa Pauni 31 milioni kunasa huduma yake ilipomsajili kutokea Benfica. Lindelof nafasi yake kwenye kikosi cha Ten Hag si muhimu sana, huku staa huyo akiwa anasumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara ambayo yamemfanya asiichezee timu yake kiasi cha kutosha.

Man United imeshafanya uamuzi wa wachezaji ambao hatawauza kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya, lakini Lindelof si mmoja wa wachezaji hao.

Man United inahitaji beki wa kati mpya kwenye dirisha hili, hivyo imeweka wazi milango ya kupokea ofa za kumhusu Lindelof, 29, ambaye amebakiza mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake huko Old Trafford.

Mabingwa hao mara 13 wa Ligi Kuu England wameshuhudia ofa yao kumsajili beki Jarrad Branthwaite ikipigwa chini huko Everton. Ofa yao ya awali ilikuwa Pauni 34 milioni pamoja na nyongeza ya Pauni 8 milioni, ambayo ilikataliwa na mabosi wa Goodison Park.

Lakini, sasa baada ya kuwa na uhakika wa kubaki kwenye kikosi cha Man United hadi msimu ujao, kocha Ten Hag anataka kuboresha timu yake kabla ya kuanza kwa msimu mpya na moja ya maeneo ambayo ametia mkazo wa kutaka usajili mpya ufanyike ni kwenye beki ya kati.

Chanzo: Mwanaspoti