Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag alalamikia soko la usajili

Skysports Erik Ten Hag Manchester United 5887807 Ten Hag alalamikia soko la usajili

Tue, 19 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag, amelaumu timu zinazopandisha bei ya wachezaji kwenye soko la usajili wakati klabu hiyo ya Old Trafford inavutiwa.

Ikiwa ni pamoja na nyongeza mbalimbali, United ilitumia zaidi ya pauni milioni 180 kununua wachezaji wanne wapya, pamoja na kumsajili Jonny Evans kwa uhamisho wa bure.

Walipolaumiwa kwa matumizi makubwa katika majira ya joto, ikilinganishwa na timu ya Brighton iliyoondoka Old Trafford Jumamosi (Septemba 16) na ushindi mnono wa 3-1, Ten Hag alipuuza.

“Nadhani timu zote zinatumia fedha nyingi” alisema.

“Hiyo ni kweli kwa klabu nyingi kama Chelsea, Liverpool, Manchester City, Arsenal, Newcastle United na hata West Ham.

“Brighton pia walitumia zaidi ya pauni milioni 80, lakini kwa hakika walileta karibu faida ya Pauni Milioni 100 katika ada za uhamisho kutoka kwa wachezaji walionunuliwa hapo awali kwa bei nafuu ambao waliwauza kwa gharama kubwa.”

“Nadhani Brighton pia walitumia fedha kama kila mtu anavyofanya. Man United inapokuja, inaongezeka bei, huo pia ni ukweli,” alisema Ten Hag alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: