Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag akipigwa chini, kulipwa pesa ndefu

Ten Hag Anajiandaa Kwa Fainali Ya Kombe La FA Bila Kujua Mustakabali Wake Ten Hag akipigwa chini, kulipwa pesa ndefu

Mon, 27 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Habari ndo hiyo. Kumfuta kazi Erik Hen Hag kutaigharimu Manchester United kulipa fidia ya Pauni 9 milioni.

Kumekuwa na ripoti kwamba zama za Mdachi huyo kuinoa Man United huenda zikaishia kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi bila kujali matokeo ya fainali ya Kombe la FA dhidi ya Manchester City uliopigwa jana Jumamosi. Tayari majina ya makocha wanne yameshaorodheshwa kwa wanaweza kumbadili kocha huyo ambao ni Mauricio Pochettino, Kieran McKenna, Thomas Tuchel na Thomas Frank. Mkataba wa Ten Hag utafika tamati Juni 2025.

Hivyo, akifutwa kazi sasa hivi, atalipwa Pauni 9 milioni sehemu ya mishahara yake iliyobaki, kama kipengele cha kushusha mshahara wake kitakuwa hakijafanya kazi kutokana na timu kushindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ten Hag, 54, mwanzoni alionekana kujiamini kwamba ataendelea kubaki kwenye kibarua chake kabla ya mambo kubadilika katika dakika za mwisho. Mwanzoni mwa mwezi huu alisema: “Kuwasiliana na Ajax? Hapana. Huko baadaye labda, inawezekana. Ni klabu inayovutia na nimekuwa na nyakati nzuri pale.”

Mshahara wa Ten Hag kwa mwezi Man United ni Pauni 750,000 na ni mmoja wa makocha wanaolipwa vizuri Ulaya. Kwa mujibu wa L’Equipe, kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone ndiye anayelipwa mshahara mkubwa zaidi kuzidi wote Ulaya, Pauni 2.42 milioni kwa mwezi. Anayefuatia ni wa Man City, Pep Guardiola anayepokea Pauni 1.66 milioni kwa mwezi.

Kocha anayeondoka Liverpool, Jurgen Klopp, alikuwa akilipwa Pauni 1.25 milioni kwa mwezi, wakati Top Five ilikuwa inakamilishwa na kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri anayelipwa Pauni 920,000 kwa mwezi.

Chanzo: Mwanaspoti