Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag ajitetea kumweka benchi Ronaldo Man United wakipigwa 6-3 za Man City

 Erik Ten Hag Ronaldo Ten Hag na Ronaldo

Mon, 3 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag amejitetea kwa kutomchezesha Cristiano Ronaldo katika mechi yao dhidi ya Manchester CityErik ten Hag anasema kuwa hakumchezesha Ronaldo katika kichapo chao cha 6-3 kutokana na heshima kwa nyota huyoNahodha wa zamani wa United Roy Keane anadai kuwa klabu hiyo inamkosea heshima Ronaldo

Ten Hag anasema hakumwingiza Cristiano Ronaldo katika mechi yao dhidi ya Manchester City kutokana na heshima kwa mshambuliaji huyo nyota.

Ronaldo alikuwa kwenye benchi katika mechi hiyo, ambayo Manchester City waliwadhalilisha majirani wao kwa kuwatandika 6-3.

Urejeo wa Marcus Rashford baada ya kupona jeraha kulimpeleka Ronaldo kwenye benchi la licha ya ten Hag kufanya mabadiliko matano katika mechi hiyo, Ronaldo hakupewa nafasi.

Alipoulizwa mbona Ronaldo hakuwa mmoja wa walioingizwa kuokoa jahazi, Ten Hag alisema kuwa ingekuwa kama matusi kwa nyota huyo kumwingiza mchezo wakati United ilikuwa tayari imezabwa 4-0.

“Sikumwingiza kutokana na heshima kwa taaluma yake kubwa. Kitu kingine, nilikuwa na nafasi ya kumleta Antony Martial. Anahitaji kucheza, lakini sitaki kulisema hivyo,” Ten Hag.

Lakini nahodha wa zamani wa Manchester United Roy Keane alikashifu jinsi inavyomfanya nahodha huyo wa Ureno na kudai kuwa klabu hiyo inamkosea heshima Ronaldo.

“Ukweli ni kwamba Ten Hag hatamchezesha Ronaldo. Inaenda kuwa mbaya msimu unavyoenda. United wamemwonyesha Ronaldo ukosefu wa heshima,” Roy Keane alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live