Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag ajipigia debe Manchester United

Erik Ten Hag Media.jpeg Ten Hag ajipigia debe Manchester United

Mon, 1 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Manchester United, Erik ten Hag amesema bosi mpya wa timu hiyo Sir Jim Ratcliffe amemhakikishia maisha na anataka kufanya naye kazi.

Wakati wa mkesha wa Krismasi, ilithibitishwa kwamba kampuni ya INEOS Group inayomilikiwa na bilionea Sir Jim Ratcliffe, ilikubali kununua asilimia 25 ya hisa za umiliki wa Man United katika dili ambalo linatarajia kukamilika mwishoni mwa Januari 2024.

Mkurugenzi wa michezo wa kampuni ya INEOS, Sir Dave Brailsford alikuwapo jukwaani uwanjani Old Trafford wakati Man United ilipotoka nyuma kwa mabao 2-0 na kushinda 3-2 dhidi ya Aston Villa kwenye Boxing Day, na Ten Hag alisema alizungumza na mabosi hao wapya.

Hatima ya Mdachi huyo ilikuwa kwenye sintofahamu kubwa baada ya ujio wa bosi mpya huku Man United ikiwa na matokeo mabaya uwanjani, ikipoteza mechi 13 tayari msimu huu.

Kocha huyo wa zamani wa Ajax, Ten Hag alisema ana uhakika atapewa sapoti kubwa na Ratcliffe ambaye inaaminika hana mpango wa kufanya mabadiliko kwa kipindi hiki. “Kama mnavyoona, mambo yamebana sana, hivyo sikuwa na muda wa kutosha kuzungumza na mmiliki mpya, lakini hilo litatokea na nalisubiri kwa hamu,” alisema Ten Hag, ambaye kikosi chake kilitarajia kumenyana na Nottingham Forest kwenye mchezo wa Ligi Kuu England usiku wa jana Jumamosi.

“Wanataka kufanya kazi na mimi. Nami nataka kufanya nao kazi. Tutazungumza kwa kina juu ya hilo, hivyo, tusubiri.”

Chanzo: Mwanaspoti