Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag ajifunza kiingereza, kujiunga na United

Talksport Erik Ten Hag Kocha wa Ajax Eric Ten Hag

Thu, 3 Mar 2022 Chanzo: eatv.tv

Moja kati ya makocha waliolengwa na klabu ya Manchester United kuchukua nafasi ya kua kocha wa kudumu kuwanoa mashetani hao wekundu Erik ten Hag sasa imearifiwa kwamba ameanza masomo ya kujifunza kuongea kiingereza kabla kufikia kwenye mazungumzo ya kuchukua mikoba ya kocha mkuu O.T.

Ten Hag anajifunza Kiingereza ili kuhakikisha anafahamu lugha hiyo kwa ufasaha kabla ya uwezekano wa kuhamia ligi kuu ya England msimu ujao. huku klabu yake ya sasa Ajax Amsterdam ikiarifu kwamba inafahamu nia ya kocha huyo kutaka kuondoka.

Mholanzi huyo anasemekana kuwa na nia ya kutaka kuhamia Manchester United mwishoni mwa msimu huu, lakini kitendo cha kujitolea kujifunza Kiingereza kwa ufasaha kitamuweka katika nafasi nzuri ya kupata nafasi sehemu nyingine ikitokea hata kama hatajiunga na united.

Vile vile imearifiwa kwambaTen Hag atakwenda na msaidizi wake Mitchel van der Gaag endapo atatimkia Uingereza. Ten Hag ni miongoni mwa wanaowania kuchukua nafasi ya Ralf Rangnick Old Trafford pamoja na Mauricio Pochettino lakini pia kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, aliyewahi kuinoa Everton na Chelsea, pia ametajwa kwenye orodha ya makocha wanaofikiriwa kupewa nafasi na mashetani hao wekundu.

Majira ya joto yaliyopita Ten Hag alipendekezwa kuwa kocha mkuu mpya wa Tottenham, hata hivyo vyanzo vya kuaminika vilidai kuwa kikwazo cha lugha kilikuwa tatizo wakati wa mazungumzo ya kufikia makubaliano.

Chanzo: eatv.tv