Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag: Tutaona

Skysports Erik Ten Hag Manchester United 5887807 Meneja wa Man United, Erik Ten Hag

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Erik ten Hag ameahidi kwamba Manchester United itajitoa kwa kila kitu ndani ya uwanja kuhakikisha inatibua mpango wa Manchester City wa kubeba mataji matatu msimu huu.

Miamba hiyo miwili itakipiga kwenye kipute cha Manchester derby cha fainali ya Kombe la FA uwanjani Wembley, Juni 3 mwaka huu.

Beki Victor Lindelof alifunga penalti ya ushindi kuwafanya Man United kutinga fainali hiyo ambapo watakwenda kipiga na Man City ya kocha Pep Guardiola. Patachimbika.

Na alipoulizwa kuhusu Man United nafasi yao ya kuichapa Man City, wanaofukuzia kuvunja rekodi yao waliyowekwa mwaka 1999 walipobeba mataji matatu, kocha Ten Hag alisema: “Tutalazimika kucheza mechi kwa usahihi.

“Ilikuwa mechi safi tulipocheza msimu huu na kuwafunga na tutakwenda kufanya hivyo tena, tunafahamu hilo. Tutajitoa kwa kila kitu na ninaposema kila kitu ni kila kitu – mashabiki wasubiri kuona hilo.

”Tutajitolea kwa kila tu kwenye taji hilo la pili, kila kitu nilichonacho, kila kitu wachezaji walichonacho, kila kitu stafu wengine walichonacho, ili kukamilisha mambo. Tunaweza, kwa sababu tumeshathibitisha hilo. Sioi rahisi kwa sababu wana timu nzuri, lakini nasi pia tuna timu nzuri.”

Shujaa wa penalti, Lindelof alisema: "Ni kitu kizuri kufunga penalti ya ushindi. Ilikuwa ahueni kubwa na tumefurahi kufika fainali. Nilijiamini, nilifahamu ni penalti ya aina gani nilihitaji kupiga na hicho ndicho nilichofanya.”

Kocha Ten Hag atakuwa na nafasi ya kushinda mataji mawili msimu huu kama chama lake la Man United litafanyikiwa kuichapa Man City katika fainali hiyo ya Kombe la FA kwa kuwa tayari wameshanyakua Kombe la Ligi msimu huu.

Man United iliwahi kuizuia Liverpool kubeba mataji matatu ndani ya msimu mmoja mwaka 1977 na imepanga kwenda kutibua mpango wa Man City, ambao kwa sasa wana nafasi ya kubeba taji la Ligi Kuu England, wametinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na wapo fainali kwenye Kombe la FA.

Kocha wa Man United, David De Gea alisema: "Bado kuna safari nzito kwenye fainali, lakini itakwenda kuwa mechi kubwa sana itakayokutanisha timu bora duniani. Tuliwaonyesha kwamba tunaweza kuwapiga Man City, acha tuamini hivyo.

"Tupo kwenye hatua sahihi. Taji moja, tumefika fainali nyingine na tunapambana kwenye Top Four. Hiyo haitoshi, ila ni hatua kubwa ukilinganisha na msimu uliopita."

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa fainali ya Kombe la FA kupigwa Juni na hii ilitokana fainali za Kombe la Dunia huko Qatar kufanyika Novemba na Desemba mwaka jana.

Man United wakati wanachukua taji lao la kwanza ambalo wameshabeba msimu huu, waliichapa Newcastle United kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Ligi. Na sasa, taji la pili watakumbana na wagumu wengine, Man City uwanjani hapo hapo Wembley.

Licha ya Man United na Man City kupata mafanikio makubwa kwenye makombe hayo ya ndani kwa miaka mingi, lakini hazijawahi kukutana kwenye mechi ya fainali na hii ni itakuwa mara ya kwanza kwao.

Kwenye Kombe la FA, ziliwahi kukutana mwaka 2011, ambapo bao pekee la kiungo Yaya Toure lilitosha kuipa Man City iliyokuwa chini ya kocha Roberto Mancini ushindi katika mchezo huo wa hatua ya nusu fainali. Man City ilikwenda kubeba ubingwa wa taji hilo, walipoichapa Stoke City 1-0, shukrani kwa bao pekee la kipindi cha pili la Yaya Toure.

Safari hii miamba hiyo imepiga hatua moja zaidi, itakutana fainali. Mambo yatakuwaje? Ngoja tuone.

Chanzo: Mwanaspoti