Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag: Sina tatizo na Varane

Raphael Varane Erik Ten Hag Manchester United Ten Hag: Sina tatizo na Varane

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag amesema kwamba hana tatizo na beki wa kati Raphael Varane na kutomjumuisha Mfaransa huyo kikosini, ni kutokana na kiwango bora alichoonyesha Harry Maguire hivi karibuni.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 inasemekana alizungumza na Ten Hag baada ya kusema hadharani kwamba ameondolewa kwenye mechi ya Manchester derby kwa sababu za kimbinu, ingawa inasemekana kuna jambo linaloendelea kati yao.

Kutokana na sintofahamu Varane amecheza mechi mbili akitokea benchi dhidi ya Fulham na Copenhagen, na inasemekana amekasirishwa na Ten Hag ndio maana akachagua kumpanga Jonny Evans na Maguire.

Uhusiano kati ya wawili hao inasemekana kuwa sio mzuri, lakini Ten Hag alipuuza akidai hakuna kitu kama hicho.

“Sio kweli, kama nilivyosema ni kuhusu sababu za busara kwa nini niliwachagua. Nadhani Maguire na Jonny walifanya vizuri. Maguire hakucheza sana mwaka jana, na nilifurahia kiwango cha Varane msimu uliopita pia,” alisema Ten Hag

Varane ana umri wa miaka 30 na kiwango chake msimu huu sio kama ilivyokuwa msimu uliopita, jambo ambalo limempa wakati mgumu Ten Hag.

Man United imeendelea kumkosa Lisandro Martinez kwani amecheza mechi sita tu tangu Aprili, mwaka huu kutokana kusumbuliwa na majeraha, hivyo Ten Hag amelazimika kuwapanga Evans na Maguire na wakati mwingine Victor Lindelof.

Wakati huohuo, Ten Hag amewaomba makocha wote wa Ligi Kuu England waitishe kikao kwa ajili ya mazungumzo na Bodi wa Waamuzi (PGMOL) kutatua masuala mbalimbali ya soka.

Chanzo: Mwanaspoti