Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag: Sihusiki kwenye suala la umiliki wa Klabu

Ten Hag 76 1140x640 Kocha wa Man United, Erik Ten Hag

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag ameweka kua hahusiki juu ya suala la umiliki wa klabu hiyo kwa namna yeyote na akili yake yeye inawaza kuhusiana na timu yake tu.

Kocha Ten Hag aliulizwa juu ya tajiri Sir Jim Ratcliffe kununua umiliki wa 25% na kocha huyo ameweka wazi akili yake haipo kwa yanayoendelea nje ya uwanja zaidi yeye anaangalia zaidi timu yake na michezo inayofuata.

Inafahamika klabu ya Manchester United ipo kwenye mchakato wa kuuzwa na wanunuaji walikua wawili na mpaka sasa amebakia mmoja, Ambapo mmoja amejitoa kutokana na kushindwana wamiliki wa sasa Familia ya Glazers.

Kocha huyo amesema suala la Sir Jim kuchukua asilimia 25 za ununuzi wa klabu hiyo linawahusu watu wa uongozi, Lakini yeye yupo makini kuangalia namna gani anaweza kuipatia matokeo katika michezo ijayo.

Kocha Ten Hag anafikiria zaidi mchezo wao unaofuata wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Sheffield United utakaopigwa kesho katika dimba la Bramall Lane, Wakitazamia kupata matokeo ya ushindi kama walivyofanya katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Brentford.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live