Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag: Sihofii kibarua changu

Erik Ten Hag Manchester United September 2023 1 Kocha wa Man United, Erik Ten Hag

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag ameeleza haogopi kibarua chake kua matatani licha ya kupoteza mchezo wa pili wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu ya Galatasaray jana usiku.

Erik Ten Hag anakiri kua wanapitia kipindi kigumu lakini kwake haoni hatari yeyote kwa kibarua chake, Kwani anaamini timu ipo pamoja na wanapambana pamoja kuanzia wachezaji, jopo la makocha na uongozi pia wa klabu hiyo.

Klabu ya Manchester United ipo kwenye hatari kubwa kwasasa kwani ina matokeo mabaya sana, Ambapo mpaka sasa wameshapoteza michezo sita kwenye michuano yote ambapo kwenye ligi ya mabingwa ulaya wamepoteza michezo miwili ya awali.

Manchester United kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo wanapoteza michezo miwili ya kwanza katika ligi ya mabingwa ulaya na mpaka wakati huu wanashika mkia kwenye kundi lao mpaka sasa wakiwa hawana alama hata moja.

Kocha Erik Ten Hag anasema anajua wako kwenye hali mbaya na hawapo kwenye ubora wao, Lakini akisema wanapaswa kufanya vizuri zaidi na kinachotakiwa ni kuweza kubadilika lakini wakati huohuo anajiamini kwenye kibarua chake kwakua uongozi unampa ushirikiano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live