Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag: Rashford anakaribia kiwango cha Mbappe

Rashford Vs Ten Hag Ten Haag na Rashford

Mon, 12 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Manchester United, United Erik Ten Hag amesema kuwa Marcus Rashford anashika nafasi ya pili baada ya Kylian Mbappe kama mchezaji bora zaidi Duniani kwa sasa.

Mshambuliaji huyo amefufua upya kiwango chake bora zaidi chini ya Mholanzi huyo msimu huu, na kumfanya aitwe tena katika kikosi cha Uingereza na kujumuishwa katika kampeni ya Kombe la Dunia.

Rashford na kikosi cha England walitinga hatua ya robo fainali dhidi ya Mbappe na Ufaransa siku ya Jumamosi, katika pambano ambalo walipoteza na kutupwa nje ya michuano hiyo

Ten Hag amesema kuwa Mbappe wakati huu ambaye ni bora kuliko yeye, wakati Rashford anaingia katika nafasi hiyo, ni mzuri na ameimarika sana na amekuwa akihusihwa na kuhamia PSG, ambapo Mbappe alisaini mkataba mpya kabla ya kampeni hii.

Mkataba wake Old Trafford unamalizika mwishoni mwa msimu huu, mshambuliaji huyo anaweza kuondoka, ingawa Ten Hag anasema wataanzisha nyongeza ya mwaka mmoja. Pia timu itaonyesha nia ya kumtaka asalie kwani ni suala la kifedha tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live