Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Hag, Guardiola watauana

Guardiola X Ten Hag Ten Hag, Guardiola watauana

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Imefichuka kuna vita ya chini chini inaendelea baina ya Manchester City na Manchester United kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi juu ya uwezekano wa kuipata saini ya staa wa Crystal Palace, Michael Olise.

Makocha wa timu zote hizi wameonekana kuvutiwa na kiwango cha staa huyu wa kimataifa wa Ufaransa ambaye mbali ya kufanya vizuri akiwa na Palace pia amekuwa na kiwango bora akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa umri chini ya miaka 21, aliyoitumikia kwenye michuano ya Euro kwa vijana mwaka jana.

Man City inamwangalia fundi huyu kama mmoja wa mastaa wanaoweza kuongeza ubora kwenye eneo lao la ushambuliaji.

Wakati huo huo, Ten Hag anataka kuanza kujenga upya kikosi chake chini tajiri Sir Jim Ratcliffe na mmoja wa mastaa anaowahitaji ni Olise.

Hata hivyo, Man City ndio inaonekana kuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kuipata saini ya fundi huyu kwa sababu staili yake ya uchezaji.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali ikiwa pamoja na The Sun na Daily Mail, Olise ambaye alikataa ofa ya kujiunga na Chelsea dirisha lililopita la majira ya kiangazi ana aina ya uchezaji ambao unafanana kabisa na jinsi Man City inavyocheza.

Kwa upande wa pesa timu zote zinaonekana kuwa na misuli ya kutosha na kwa mujibu wa ripoti Palace inahitaji zaidi ya Pauni 60 milioni ili kumuuza.

Msimu huu amecheza mechi 11 za michuano yote.

Chanzo: Mwanaspoti