Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Haag apandisha presha wachezaji Man United

Skysports Erik Ten Hag Manchester United 5887807 Kocha wa Manchester United Eric Ten Haag

Thu, 10 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Manchester United Eric Ten Haag ameweka wazi anafikia kuingia sokoni na kutafuta beki mpya wa kulia kwa ajili ya kutoa ushindani wa namba kwa mabeki wa kulia waliopo klabuni hapo.

Ndani ya klabu ya Manchester United kuna mabeki wawili wa kulia lakini mmoja ndio anaonekana kufanya vizuri na kuimarika kwa kiwango, na kocha wa klabu hiyo anatambua kuimarika kwa kiwango cha beki Diogo Dalot lakini anahitaji beki mwingine kwajili ya kuleta ushindani kikosini pamoja uwepo wa michuano mingi.

Beki mwingine wa klabu hiyo Aaron Wan Bissaka anaonekana ni wazi hayupo kwenye mipango ya mwalimu Ten Haag kutokana na ufinyu wa nafasi ambao amekua akiupata klabuni hapo tangu kuwasili kwa mwalimu huyo majira ya joto.

Huku ikielezwa Man United wanatafuta namna ya kumalizana na Wan Bissaka ili kuachia nafasi ya kuweza kusajili beki mwingine wa kulia klabuni hapo.

Mwalimu Eric Ten Haag inaelezwa alivutiwa na beki wa Barcelona aliepo kwa mkopo klabu ya Ac Milan Sergino Dest katika majira ya joto lakini ndani ya dirisha dogo haiwezekani tena, Hivo inabidi kutafuta beki mwingine mbadala na kuweza kumsajili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live