Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ten Haag amtaka Maguire wa England

England Defender Harry Maguire Mlinzi wa England na Man United, Harry Maguire

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Manchester United Erik ten Haag, amemtaka Harry Maguire kuendeleza kiwango chake cha Timu ya Taifa akiwa na United ili kupambana kurejea kwenye kikosi cha Mashetani Wekundu.

Maguire alianza mechi tatu pekee za Ligi ya Primia kwa United msimu huu kabla ya kwenda Kombe la Dunia akiwa na England na kuonekana katika michezo yote mitano katika kufuzu kwa robo fainali.

Gareth Southgate amerudia kumuunga mkono beki huyo wa kati kwenye hatua ya Kimataifa, ingawa Raphael Varane na Lisandro Martinez wamekuwa washirika wa Ten Hag wanaopendelewa na United msimu huu.

Baada ya Uingereza kuondolewa na Ufaransa siku ya Jumamosi, Ten Hag anatumai Maguire anaweza kurejea Old Trafford kwa kujiamini kutokana na uchezaji wake wa kuvutia akiwa Qatar.

Ten Haga maesema kuwa; “Ninaweza tu kumuunga mkono. Nimeulizwa mara nyingi kama anatosha kunichezea na ni wazi anatosha kucheza katika kiwango cha juu, na kisha ni juu yake kuonyesha ujasiri huo uwanjani na hakuonyesha hivyo katika mechi zote za United.”

Kocha huyo aliendelea kusema beki huyo anapocheza kwa kujiamini kama sasa, yeye ni mchezaji muhimu sana kwao na ndivyo kila myu anatarajia. Na hicho ndicho ambacho Maguire anatarajia kutoka kwake kutokana na kuwa na kiwango cha juu zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live