Kocha wa Manchester United Eric Ten Haag ameongea na waandishi wa habari leo hii kuelekea mchezo wao wa jumamosi dhidi ya klabu ya Chelsea na kusema ni anasimamia maadili na nidhamu klabuni hapo.
Kocha huyo amefunguka baada ya sintofahamu iliotokea jumatano katika mchezo kati ya Manchester United na Tottenham Hotspurs ambapo nyota wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo aliondoka uwanjani kabla ya mtanange huo kumalizika na kuibua mjadala mkubwa.
Ronaldo aliondoka uwanjani katika mchezo huo kabla ya mchezo kumalizika kutokana na kutopata nafasi ya kucheza akionesha kukasirishwa na kitendo hicho huku klabu hiyo ikitoa taarifa ya kumsimamisha mchezaji huyo na hatakuepo katika mchezo dhidi ya Chelsea.
Katika mkutano huo kocha huyo amezungumza juu ya sakata hilo “Ninawajibika kwa utamaduni, Lazima niweke viwango kwenye maadili. Soka ni mchezo wa timu. Lazima uweke kiwango Fulani” Alisema Ten Haag.
Kutokana na maelezo hayo ni wazi kocha huyo hakufurahishwa na kitendo alichokifanya Ronaldo cha utovu wa nidhamu na taarifa ya kumsimamisha staa huyo ni wazi ni katika hali ya yeye kusimamia misingi ya maadili na nidhamu klabuni hapo kama alivyosema.
Pia kocha huyo ameeleza kua mchezaji huyo aligoma kuingia uwanjani pale alipohitajika na sio kama ambavyo watu wengi wanatafsiri kua alinyimwa nafasi ya kucheza katika mchezo huo.
“Ndiyo Ronaldo alikataa kuingia uwanjani dhidi ya Tottenham. Ni lazima kuwe na matokeo. Ni muhimu kwa mtazamo na mawazo ya kikundi” Alisema Ten Haag.
Kutokana na maelezo ya kocha huyo imeonesha staa huyo hakutaka kuingia uwanjani kwa wakati ambao alitakiwa kuingia huku sababu ikiwa haijawekwa wazi, Lakini kutokana na mchezo ulivyokua ukiendelea ni wazi staa huyo hakua tayari kuingia uwanjani kutokana na dakika zilizobaki katika mchezo huo.
Maelezo ya kocha wa klabu hiyo yameeka ukweli wazi ambapo mashabiki wengi wa klabu hiyo wakifikiri kocha huyo anamdharau mchezaji huyo jambo ambalo sio sahihi kwa mujibu wa kocha huyo.