Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tembo kazi imeanza Uturuki

Tembo Warriors 1 Game Tembo kazi imeanza Uturuki

Sat, 1 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha timu ya taifa ya soka la walemavu, Tembo Warriors leo mchana itatupa karata ya kwanza kwenye Fainali za Kombe la Dunia itakapoikabili Hispania katika mechi ya kwanza ya Kundi E itakayopigwa kwenye mji wa Pendik uliopo jijini Instabul, Uturuki kunakofanyikia fainali hizo.

Tembo ipo nchini Uturuki kwa karibu mwezi mzima kwa ufadhili wa serikali kwa ajili ya fainali hizo inazozicheza kwa mara ya kwanza na kucheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Angola na Morocco.

Kocha mkuu, Salvatory Edward alisema; “Wachezaji wote wapo fiti kwa mchezo huo na wala hakuna majeruhi hadi sasa, hivyo kwa hakika kila kitu kimeenda vizuri kwenye uwanja wa mazoezi na sasa ni kujipanga kwa mchezo huo ili kuvuka makundi,” alisema Edward anayesaidiana na Ivo Mapunda. Nahodha wa kikosi hicho Juma Kidevu alisema ndoto yao ni kuanza na kumaliza vyema mashindano hayo na kwamba watapambana kuipeperusha vyema bendera ya taifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live