Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tembo Warriors watoka patupu Misri

Tembo Warriors Ulayaaa Tembo Warriors.

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Timu ya Taifa ya mpira wa miguu kwa watu wenye Ulemavu Tanzania ‘Tembo Warriors’ wameshindwa kufikia malengo ya kutafuta nafasi ya kufuzu ya kucheza Kombe la Dunia, 2026.

Tembo Warriors walishindwa kutafuta tiketi hiyo juzi baada ya kupoteza mechi ya kusaka nafasi ya saba katika michuano ya Afrika (AAFCON) kwa kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya wenyeji wa mashindano hayo Misri.

Kikosi hicho kinatarajia kurejea nchini Alhamisi Juni 30, baada ya fainali hizo za Afrika kumalizika jana.

Akizungumza na Nipashe jana, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Salvatory Edward alisema vijana wake walipambana lakini haikuwa bahati kwao na sasa wanarejea kujipanga kwa msimu mwingine.

Alisema wanasikitika hawakufikia malengo ya kucheza fainali za Afrika na kushindwa kutafuta tiketi ya kuwa miongoni mwa timu saba zitakazoshiriki Kombe la Dunia.

“Tumepoteza vyote tunarejea nyumbani kujipanga kwa wakati mwingine, mashindano yalikuwa mazuri wachezaji walipambana na tunakiri kuna sehemu tulizidiwa.

Malengo yetu yalikuwa kucheza fainali za Afrika tukashindwa kwa kuondolewa robo fainali na tukawa na nafasi ya kutafuta mshindi wa saba ili tuweze kufuzu Kombe la Dunia lakini tumepoteza dhidi ya Misri,” alisema kocha huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live