Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tegete amgomea Grant, aipa Stars matumaini

Taifa Stars AFCON Vazi Tegete amgomea Grant, aipa Stars matumaini

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkongwe nchini, John Tegete amesema watu hawapaswi kuibeza timu ya taifa ‘Taifa Stars’ licha ya kupangwa kundi gumu kwenye Kombe la Mataifa Afrika (AFCON), linaloendelea nchini Ivory Coast, huku akiamini Stars itashinda mechi mbili kwenye kundi hilo.

Taifa Stars iko kundi F, pamoja na timu za taifa za Morocco, DR Congo na Zambia na itacheza mchezo wake wa kwanza leo dhidi ya Morocco, kabla ya kumenyana na DR Congo na kumalizana na Zambia.

Tegete ambaye kwa sasa anainoa Mwadui FC alitoa kauli hiyo katika mahojiano na Mwanaspoti jijini hapa baada ya kocha wa zamani wa Chelsea, Avram Grant ambaye anaifundisha timu ya taifa ya Zambia kudai kuwa katika kundi lake timu zinazomuumiza kichwa ni Morocco na DR Congo na siyo Taifa Stars.

Tegete alisema hana wasiwasi na kikosi cha Tanzania kwani kwa sasa kina mchanganyiko wa vipaji kutoka ndani na nje ya nchi pamoja na uzoefu huku akitamba kuwa Stars ina uwezo wa kuvuna pointi sita katika kundi F zikiwemo tatu mbele ya Zambia inayofundishwa na Grant.

“Katika timu ambazo mimi naona tunaweza kuifanyia vitu ambavyo tunatakiwa tushinde mojawapo ni Zambia, leo naongea hapa keshokutwa utaniuliza, Zambia hii siyo ile kila kitu kinakwenda na wakati hawana kizazi cha kutisha kama zamani, kwa sasa hatupishani sana viwango vya wachezaji tena wasijidanganye watakuja kulia,”

“Mimi najua kuna timu mbili hivi tutazifunga, mimi sidhani kama tutafanya vibaya kuna timu kama mbili hivi tutazifunga kwa sababu na sisi tuna wachezaji wazuri wenye uzoefu na wengi wanacheza nje ya nchi hii nayo ni faida kwa timu kwa sababu ni muunganiko mzuri sana, sasa kinachohitajika pale kwanza ni wachezaji kujitoa kwa ajili ya taifa lao,”

“Na sisi tuna wachezaji wazuri wenye uzoefu na wengi wanacheza nje ya nchi hii nayo ni faida kwa timu kwa sababu ni muunganiko mzuri sana, sasa kinachohitajika pale kwanza ni wachezaji kujitoa kwa ajili ya taifa lao. Pili, kila mmoja kujituma, siyo lazima awamu hii tufike hatua za juu lakini angalau tukivuka hatua hizi za mwanzo ni sifa kwa nchi,” alisema Tegete

Chanzo: www.tanzaniaweb.live