Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tegete aipeleka Yanga fainali Caf

Yanga Win Nigeria Ll Wachezaji wa Yanga

Sat, 29 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha mkongwe nchini, John Tegete amesema kama Yanga wakiongeza kasi kidogo basi msimu huu itatinga fainali ya Kombe ya Kombe la Shirikisho Afrika na kuwashangaza wengi ambao hawaipi nafasi kubwa kufika hatua hiyo.

Yanga itarudiana na Rivers United katika mchezo utakaochezwa kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa ambapo mechi ya kwanza iliyopigwa nchini Nigeria timu hiyo ilishinda 2-0.

Timu hiyo inahitaji ushindi au sare yoyote katika mchezo huo wa marudiano kufuzu hatua ya nusu fainali ambapo watakutana na mshindi wa mchezo kati ya Pyramids ya Misri au Malumo Gallants kutoka Afrika Kusini.

Akizungumza Tegete alisema kwa ubora wa Yanga kwa sasa anaiona kabisa itafika fainali ya Kombe la Shirikisho iwapo watakomaa katika mchezo wao wa marudiano na Rivers kisha kujipanga kwenye nusu fainali.

Alisema kwa sasa Yanga imekuwa bora sana hivyo iwapo watafuzu nusu fainali anaona kabisa anaweza kukutana na yoyote kati ya Pyramids au Malumo na kuwafunga kwani ameziona timu hizo mbili zinafungika kirahisi.

Tegete alisema kinachotakiwa kwa wachezaji ni kujiandaa kwa kila mchezo watakaocheza na pia kuwa na nidhamu kubwa ya mechi zote watakazocheza za nyumbani na ugenini ambapo wakifanya hivyo basi msimu huu wataweka rekodi ya kucheza fainali.

"Niliangalia mchezo wa Pyramids na Malumo ambao walitoka sare ya 1-1 nimeona si timu za kutisha sana haswa kwa Yanga hii ya sasa naamini kabisa akikutana na mmoja wapo atamtandika vizuri tu,’’ alisema Tegete na kuongeza;

“Kinachotakiwa kwa sasa ni Yanga kuhakikisha wanafanya vizuri mchezo huu wa marudiano dhidi ya Rivers na kufuzu nusu fainali kikubwa ni kuwaheshimu wapinzani wao wasiwadharau kwa kuwa waliwafunga kwao.’’

Chanzo: Mwanaspoti