Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tegete afichua mipango mipya

Tegere Pc Aliyekuwa mshambuliaji wa Pamba, Jerry Tegete

Fri, 30 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Aliyekuwa mshambuliaji wa Pamba, Jerry Tegete amesema licha ya mkataba wake kumalizika na kikosi hicho ila bado anaendelea kujiimarisha zaidi kwani malengo yake ni kuendelea kucheza msimu ujao.

Nyota huyo wa zamani wa Yanga alisema licha ya kutofikia malengo ya kuipandisha timu hiyo kwenda Ligi Kuu Bara ila haimfanyi kuachana na soka kwani anaamini umri unamruhusu kuendelea kucheza.

"Niliumia sana baada ya kushindwa kuipandisha Pamba Ligi Kuu Bara lakini ndio mpira wa miguu ulivyo, kwa sasa naendelea na mazoezi binafsi ya kujiweka fiti kwani nahitaji kucheza," alisema.

Kwa upande wa Kocha wa timu hiyo, Yusuf Chippo alisema licha ya mchezaji huyo kumsajili dirisha dogo la Januari mwaka huu ila aliongeza ufanisi kwenye kikosi hicho.

"Ukimuangalia unamuona bado ni mchezaji ambaye anapenda ushindani na hata alivyokuja hapa kuna kitu kikubwa alikiongeza hususani uzoefu wake kwa kushirikiana na vijana wadogo waliopo hapa."

Tegete ambaye aliwika akiwa na Yanga na Taifa Stars alijiunga na Pamba akitokea African Lyon baada ya kukaa nje ya uwanja kwa miezi

Chanzo: Mwanaspoti