Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tegemea kuiona Simba mpya kesho - Matola

Matola: Bado Tuna Matumaini Ya Kufanya Vizuri Ligi Kuu Tegemea kuiona Simba mpya kesho - Matola

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mchezo wa kesho Kocha Msaidizi Simba SC ,Seleman Matola amesema hawapo tayari kupoteza mchezo wa kesho licha ya kuwepo kwa mfululizo wa matokeo mabaya hivi karibuni kwa upande wao.

“Hii ni mechi nyingine hatuangalii kilichotokea nyuma tunaangalia mchezo wetu wa mbele. Kitu kizuri tuna wachezaji wenye uzoefu kwa upande wetu sisi hii haitakuwa derby nyepesi “

“Hatukuwa na matokeo mazuri katika mechi zilizopita lakini hatutakubali kupoteza katika mechi zetu zijazo hasa katika mchezo na Young Africans, tunahitaji kupata ushindi.”

“Wachezaji wapo fiti na wana morali ya kutosha kwa mchezo huo kwani lengo letu ni kupata ushindi. Benchi la ufundi linaendelea kurekebisha mapungufu ili timu iwe na makali ya hali ya juu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live