Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tchouameni apania Real Madrid

F7561234 556C 42C1 8B6F 33087F713F87.jpeg Aurelien Tchouameni

Tue, 21 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Aurelien Tchouameni amekua akipitia kipindi kigumu kwenye klabu ya Real Madrid lakini inaelezwa hajakata tamaa na ataendelea kupambana zaidi.

Tchouameni anaonekana kupoteza nafasi ndani ya kikosi cha Real Madrid baada ya kupata majeraha mapema baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia, Taarifa zinaeleza mchezaji huyo anachukulia hali hiyo kama sehemu ya mapito lakini anaweza kurudi na kuanza kufanya vizuri.

Kiungo huyo ambaye amejiunga na klabu ya Real Madrid kwenye dirisha kubwa lililopita akitokea Monaco, Huku kukiwa na matarajio makubwa kutoka kwake kuchukua nafasi ya Carlos Casemiro aliyetimkia klabu ya Manchester United lakini kwasasa anaonekana kupoteza nafasi.

Eduardo Camavinga ambaye ni raia wa kimataifa wa Ufaransa anaonekana kuchukua nafasi ya kiungo mwenzake Tchouameni kwenye kikosi cha Real Madrid, Lakini Aurelien amejikita kwenye kujituma zaidi ili kuweza kurudisha nafasi yake kwenye kikosi cha Carlo Ancelotti.

Aurelien Tchouameni hawazi suala la kukata tamaa wala kutupa taulo ulingoni kama ambavyo imekua kwa wachezaji wengine wanapopoteza nafasi kwenye timu, Lakini mchezaji huyo anaamini hatawaangusha mashabiki wa klabu hiyo kwani atarudi kwa nguvu na kuanza kufanya vizuri na kufurahisha mashabiki wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live