Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tchakei, Rupia wagombaniwa

Rupia Mdk Tchakei, Rupia wagombaniwa

Thu, 20 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Singida Black Stars, imesema kuwa imepata ofa nyingi kutoka timu mbalimbali nchini zikiwahitaji wachezaji wake, straika Elvis Rupia, raia wa Kenya na kiungo mshambuliaji wa Togo, Marouf Tchakei.

Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo, ambayo zamani ikiitwa Ihefu, Muhibu Kanu, amesema, mbali na wachezaji hao, pia kuna kiungo mkabaji, Yusuph Kagoma ambaye kuna timu inamhitaji.

"Kuna ofa nyingi mezani, nimeiona ya Rupia kuna watu wametuma barua ya kuleta ofa, zipo mezani kwangu nimeziona kuna wanaomhitaji Tchakei kuna timu inamtaka Yusuph Kagoma, yaani klabu zinataka wachezaji wetu tofauti tofauti," alisema Kanu.

Mkurugenzi huyo amesema hakuna mchezaji asiyeuzwa na klabu yoyote itakayofuata utaratibu, basi hawana matatizo, kwani na wao watakwenda kusaka wachezaji wengine bora zaidi.

"Kama ni kuondoka sawa, kwa sababu hakuna mchezaji asiyeuzwa, kinachotakiwa ni makubaliano ya timu mbili, tutauza wanaohitajika na klabu zingine na kupata dau nono, tutazuia wale ambao kocha atasema anawahitaji, na pia na sisi tutasajili kutoka klabu zingine," alisema.

Taarifa za ndani kutoka klabu hiyo zinaeleza Simba inawahitaji wachezaji wawili, ambao ni Kagoma ambaye tayari wameshamalizana na Wekundu wa Msimbazi, na sasa kinachosubiriwa ni dau kwenye klabu yake, na Tchakei ambaye ilimkosa kipindi cha dirisha dogo la usajili msimu uliomalizika.

Wakati huo huo, kikosi cha Singida Black Stars, kinatarajiwa kuanza maandalizi ya msimu mpya (pre season), Julai 3, mwaka huu.

Kanu, alisema uongozi umeshaweka malengo yake, ukitaka maandalizi ya msimu yaanze mwanzoni mwa mwezi ujao, huku ukimuachia kocha wake mpya, Patrick Aussems, kuchagua sehemu anayotaka kuweka kambi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live