Mtangazaji na Mchambuzi maarufu wa soka katika Ligi ya England Martin Tyler (77), anatarajia kuondoka Sky Sports baada ya kulitumikia shirika hilo kwa miaka 33.
Tyler ni mmoja wa watangazaji ambao sauti zao ni maarufu sana nchini England na duniani kwani amekuwa mchambuzi kiongozi kwenye Shirika la Sky Sports kwa kila msimu wa Ligi ya England tangu kuanza kwake mwaka 1992.
Mchambuzi huyo hastaafu bali anaondoka Skysports kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa 2023-24. ”Imekuwa ni fursa nzuri sana kuchangia historia ya utangazaji katika Ligi kubwa zaidi duniani”
"Nimefanya kazi na wataalamu wengi katika sekta ya televisheni. Ninawashukuru wote kwa ushirikiano. Imekuwa heshima kubwa kuwa sehemu ya timu yenye vipaji.”
Tyler aliyewahi kufanya kazi na ITV mwaka 1974, alijiunga na British Satellite Broadcasting mwaka 1990 kampuni ambayo ilijiunga na Sky baadaye mwaka huo huo.