Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tatizo ni Kocha au wachezaji Man United?

Ten Hag X Onana Tatizo ni Kocha au wachezaji Man United?

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mpira wa miguu ni mchezo wa timu, Wachezaji wanaocheza maeneo tofauti ndani ya uwanja hufanya kazi pamoja ili kuweza kushinda mechi. Safu ya ulinzi, safu ya kiungo na safu ya ushambuliaji zote zinatakiwa kufanya kazi kwa pamoja ili kupata matokeo chanya kiwanjani.

Haya yote hutengenezwa na Kocha na benchi lake la ufundi, Kocha atapendekeza Wachezaji anaowahitaji kulingana na Falsafa zake ili aweze kukifanya kile kilicho kichwani kwake kifanyiwe kazi ndani ya uwanja. Kocha ndiye anayetengeneza mpango jinsi gani anataka timu yake icheze inapokua na mpira na isipokua na mpira.

Makocha wa kisasa Wanapenda kucheza kimbinu zaidi na matumizi ya nguvu sambamba na kasi, hii inasababishwa na mpira kubadilika Wachezaji Wavivu hawana nafasi tena zama hizi.

Nimeitizama timu ya Manchester United msimu huu timu inapoteza dira kila kukicha,Eric Ten Hag anakazi ya kufanya maana timu kwa sasa haieleweki kitu gani inafanya ndani ya uwanja, Wachezaji wanacheza kama hawafahamu maelekezo ya Mwalimu, timu haina madhara isipokua na mpira kwenye kupeleka presha kwa Wapinzani na inapokua na mpira kwenye ujenzi wa mashambulizi haieleweki jinsi gani inashambulia.

Manchester United inamchezaji mmoja mmoja lakini haina timu ya kushinda mechi ya mpira wa miguu, unahitaji utulivu kuanzia kwenye Uongozi ili timu iweze kufanya vizuri ndani ya uwanja.

Johan Lange huyu ndiye aliyependekeza jina la Ange Postecoglu akiwa anafundisha Glascow Celtic ya Scotland,najua Watu wengi Watakua Wamemfahamu kwa kazi anayoifanya Spurs, huyu Johan Lange ndiye aliyeijenga hii Aston Villa ya Unai Emery. Mkurugenzi wa ufundi Kijana anayefanya vizuri kwa sasa barani Ulaya.

Ukiwa na Mkurugenzi wa ufundi mzuri husaidia kung'amua falsafa sahihi ya timu, Kocha ambaye ataishi kwenye hiyo falsafa na husajili Wachezaji ambao Wataitafusiri vizuri falsafa husika.

United inahitaji kufanya mabadiliko kuanzia kwenye uongozi ili iweze kufanya vizuri uwanjani, Mkurugenzi wa ufundi Kijana ambaye ataweza kuanzisha projekti mpya ya klabu, kwa sasa Eric Ten Hag ameshagonga mwamba hakuna kipya atakachoweza kuongeza kwenye timu.

Timu inamchezaji mmoja mmoja ila haichezi kitimu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live