Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tatizo la washambuliaji ni pasua kichwa Afrika

Sankara Karamoko Yanga.jpeg Tatizo la washambuliaji ni pasua kichwa Afrika

Wed, 29 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sankara Karamoko aliondoka kwenye Klabu ya ASEC Mimosas timu ikiwa hatua ya makundi, aliikosa michezo miwili ya mwisho.

Kipindi hicho alikuwa ameshafunga mabao manne kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Tangu alipoondoka, michezo nane imechezwa (miwili ya mwisho hatua ya makundi, miwili robo fainali, miwili nusu fainali na miwili fainali) lakini hakuna mchezaji aliyefunga mabao kumzidi yeye au hata kumfikia (mabao manne).

Mahmoud Kahraba wa Al Ahly ndiye mchezaji ambaye amecheza michezo mingi akiwa na nafasi ya kumpiku Karamoko, lakini ameishia mabao matatu tu.

Mchezaji kuwa na idadi ndogo ya mabao (manne) kwenye mashindano yenye michezo mingi (kumi na mbili) tafsiri yake ni kwamba Ligi nyingi za Afrika zina changamoto ya ufungaji, kinyume chake ni kwamba timu za Afrika zina safu nzuri ya ulinzi, yaan timu zinaingia uwanjani zikiwa na lengo namba moja kutoruhusu bao badala ya kujiwekea lengo la kufunga mabao mengi zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live