Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tatizo la Yanga sio ufupi wa wachezaji - Edo

Job Kibwana Edo Kumwembe

Tue, 14 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi na mwandishi nguli wa michezo nchini, Edo Kumwembe amesema kuwa kilichowaponza Yanga kufungwa na US Monastir huko Tuninia sio ufupi wa mabeki wao bali ni kushindwa kufanya 'marking' nzuri kwa wapinzani wao hasa wakati wa kupigwa kwa mipira iliyokufa 'set pieces'.

Edo amesema hayo kufuatia mjadala mkubwa kuibuka mitandaoni baada ya Yanga kukubali kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Waarabu hao huku mabao yote yakifungwa kwa vichwa kutokana na mipira iliyokufa.

Aidha, Edo amesema kuwa mabao waliofungwa Yanga kwenye mchezo huo wa Kundi D wa Kombe la Shirikisho Afrika, hakuna tofauti na bao ambalo Simba walifungwa na Horoya kule Guinea katika Kundi C la Kombe la Mabingwa Afrika.

"Yanga wamefungwa bao la kwanza kwa mpira wa adhabu, wakafungwa la pili kwa free header mpira wa kona. Simba juzi (Jumapili) walifungwa kwa free header ya kona.

"Simba walipocheza na Kaizer Johannesburg walifungwa manne huku mabao matatu yakiwa ya kichwa, hatufanyi marking za uhakika katika boksi, tatizo sio urefu wala ufupi, tatizo ni marking na disturbance kwa adui.

"Ingekuwa hivyo Peter Crouch angekuwa anafunga kila kona. Marking za wenzetu ni vurugu mpaka mwamuzi anasimamisha mchezo.

"Header za juzi na na jana (Jumapili) wapigaji wamekaa nyuma kabisa kukwepa disturbance za pale katikati na wala hawakuruka na mtu. Poor marking and lack of concentration," amesema Edo Kumwembe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live