Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tatizo la Simba lilianzia hapa - Julio

Julio: Simba SC Imezingua Sana Kwa Mgunda Mgunda na Robertinho.

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Klabu ya Singida Fountain Gate FC, Jamhuri Kiwelu (Julio) amesema kuwa tatizo la kikosi cha Klabu ya Simba lilianza tangu wakati wa pre-season mzimu uliopita.

Julio ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba amesema hayo baada ya Simba kukubali kichapo kingine cha bao 2-1 kutoka kwa watani zao yanga kwenye mchezo uliopigwa juzi Aprili 20, katika Dimba la Mkapa.

“Simba tatizo lao lilianzia pre-season. Kocha Mgunda alikuwa ameshatengeneza mfumo mzuri, alipokuja Robertinho akaanzia katikati ya msimu, akaenda na mfumo wa Mgunda, lakini msimu ulipoisha timu ikaenda pre-season Uturuki lakini kocha akaiacha timu akaenda kwao, hata wachezaji walienda pre-season kwa mafungu, kwa hiyo muda wa kutengeneza combination ya wachezaji wapya na wa zamani haukuwepo.

“Benchikha amekuja katikati ya msimu kwenye dirisha dogo akafanya usajili, lakini wachezaji wengi walikuwa wameitwa timu ya Taifa kwa ajili ya AFCON, kwa hiyo nay eye hakupata muda wa kutengeneza muunganiko mzuri wa wachezaji, ndiyo maana timu ime-collapse. Yanga wanajituma na wana kikosi kipana ndiyo maana wanafanya wanayoyafanya,” amesema Julio.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live