Yanga ya sasa inaubonda kweli kweli, unamiliki mchezo, inafunga mabao, lakini sharti ni kupitia first eleven yao ambayo imekuwa ni kama ya kudumu, pindi inapotokea mabadiliko kadhaa tena kuanzia namba 6 na kuendelea hakika hulioni tishio tena la Yanga katika eneo hilo.
Tafsiri yake kuna changamoto kwa wachezaji ambao wanapaswa kuingia kwa ajili kufanya kazi ya ziada katika kuhakikisha kilicho bora kinapatikana.
Moja ya sifa ya Yanga ya misimu miwili iliyopita ni kikosi chake cha kwanza kutotabirika, ni maeneo machache sana ambayo Nassredine Nabi alikua hayagusi katika kikosi cha kwanza.
Eneo la langoni Djigui Diarra, kiungo wa kati Khalid Aucho na mshambuliaji Fiston Mayele, lakini maeneo mengi kulikua na rotation kulingana na mahitaji ya kiufundi ya kocha na kiuhalisia kila mchezaji alikua anaonyesha tija kadri alivyokuwa akipewa nafasi.
Kwa sasa huwaoni tena kina Farid Mussa, Sure Boy, Kibwana Shomari, na mbaya zaidi huwaoni waliotarajiwa pengine wangeongeza depth kikosini kama Gift Fredy, Skudu Makudubela, Jonas Mkude, Hafiz Konkoni n.k, hawana cha ziada na hata wakipewa nafasi huoni faida ya moja kwa moja.
Maswali ni je, kwa nini katika era ya Nassredine Nabi kila mchezaji alikuwa ana-show up pindi anapowewa nafasi?
Je, kipi kimebadilika hivi sasa? Katika makaratasi Yanga inaonekana kuwa na kikosi kipana lakini ndani ya Uwanja Yanga wana kikosi finyu na ni hatari kwa timu yenye mashindano mengi tena yenye malengo makubwa ya kuyafikia, dirisha la usajili ndio hilo hapo.