Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tatizo Simba ni uongozi - Hans Rafael

Hans Rafael Tatizo Simba ni uongozi - Hans Rafael

Tue, 9 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka Bongo Hans Rafael amesema tatizo linalosababisha Simba SC ishindwe kufanya vizuri ni uongozi kushindwa kutimiza majukumu yao vizuri.

Amesema viongozi hawachukui maamuzi sahihi kwenye madirisha ya usajili na ndio maana hukosea kwa kupata wachezaji wasiokuwa na sifa.

“Ukiitazama Simba unaona hawana ‘future’ lakini kuna wachezaji wengi sana Simba ilibidi iwasajili lakini viongozi hawakuchukua maamuzi sahihi kuwasajili badala yake wakaenda kuwasajili kina Duncan Nyoni, Sawadogo, Okwah n.k”

“Shida kubwa Simba sio wachezaji bali ni uongozi wao haufanyi vitu sawasawa na wanabidi kubadilika haina haja kusajili wachezaji 10 dirisha moja badala usajili wachezaji watatu wenye ubora wa juu kisha usubiri dirisha linalofuatia usajili Wachezaji wengine wawili maana Timu haijengwi kwa msimu mmoja,” alisema Hans.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live