Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tarimba awapiga kijembe Simba

Tarimbaaa Mbunge wa Kinondoni Abbas Tarimba

Fri, 4 Feb 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mbunge wa Kinondoni Abbas Tarimba amesifia ushindi wa Simba bungeni akiwataka kuendelea na moto huo.

Tarimba ambaye ni mpenzi wa timu ya Yanga ametoa pongezi hizo ndani ya bunge leo alipouliza swali la nyongeza lakini alilenga kumtania mbunge wa Ilala Mussa Zungu.

Simba ilicheza jana na Timu ya Tanzania Prison katika uwanja wa Benjamin Mkapa na kuvuna pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Meddie Kagere kwa mkwaju wa penalti.

Hata hivyo Zungu aliamua kunyamaza bila kumjibu mbunge huyo ambaye wanatoka mkoa mmoja lakini alicheka.

"Nakupongeza mheshimiwa Mwenyekiti jana Simba mlishinda, tunaomba muendelee na moto huo, nadhani umenielewa Mwenyekiti," amesema Tarimba huku akipigiwa makofi na wabunge mashabiki wa Yanga.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz